Skippa Mistari – Mpaka lini Lyrics

INTRO: 
Jyeeah, (aha aha)
Skippa Mistari, (jyeah jyeah)

Niko na stress yani, (mob sana)
Nahauntiwa na past (ebu imagine)
Sina hopes na future (we fikiria)
Niko stuck in the present (aha)
Thats why nauliza, (aha)
Mpaka lini ah
mpaka lini ah
mpaka lini mpaka lini mpaka lini ah! 

CHORUS LYRICS: 
kila siku nina stress, ju mi ninawaza
nashika mic, sauti ninapaza
jana kesho leo, swali moja nauliza
mpaka lini, ah, mpaka lini, ah! 

VERSE 1 LYRICS:
sifikirii poa juu mawazo yamenibana
votia MP wangu poa but saa hii amenikana
akitafuta kura ndio mwisho mtaani kupatikana
ata simu kajaribu, mteja wa nambari hawezi patikana
ninakumbwa na dhiki ju malengo sijaafiki
angalia mtaani venye shida zimejaa
sewage zinaleak barabara hazipitiki
yote kwa sababu, maMP wanafiki walijidai marafiki
tuwape kura fifty wakalie hiyo kiti
sa kusema ukweli hakuna kitu wanado
kwa bunge wanalala na kusnore kama chura
CDF wanakula ndio maana tumbo wamefura
shule ndio nilipita but kazi sijapata
nazidi tapatapa ka mtoto wa bata
polisi nao daily ni risasi wanatupa. 

CHORUS LYRICS: 
kila siku nina stress, ju mi ninawaza
nashika mic, sauti ninapaza
jana kesho leo, swali moja nauliza
mpaka lini, ah, mpaka lini, ah! 

VERSE 2 LYRICS:
maswali ya polisi
wakora ndani ya jiji
ingia kanisani, patana na kasisi
mlafi shinda fisi
badala ya kutuombea, 
mikono ekelea na mapepo kukemea
ni nini wanado?
namba ya ZAP na MPESA ndio wanazidi kutupea
na hatuna hiyo pesa juu umaskini watutesa
nishagundua siri, kabila huku mbili
maskini na tajiri, viongozi na wafuasi, mahustler na masonko
ndio kisa na maana
wenye nchi wana GUCCI, wananchi wako UCHI
nchi yetu ya Kenya kama shamba la wanyama
bila ufisadi hauwezi ukapenya
mahater kusengenya fans pia wanapirate
wananchi twaugua njaa pia kutuua
kusota na kukonda ni mishipi tunakaza. 

CHORUS LYRICS: 
kila siku nina stress, ju mi ninawaza
nashika mic, sauti ninapaza
jana kesho leo, swali moja nauliza
mpaka lini, ah, mpaka lini, ah! 

VERSE 3 LYRICS:
ka me ni msanii, mi ni kioo cha jamii
nafaa kuspit kile me ninasee si kile ninafeel
kwa jina ni Skippa, ongeza Mistari
nazidi tafakari kiandika hizi mistari
tembea kila mahali kutafuta hii mali
ata ka mdosi mkali
chakula pia ghali
nimesota sina mali
naugua sina hali
hakuna dawa hospitali
ntatoboa siri kali
nichongoe serikali
nimekam na silaha
nimekam kama jeshi
microfoni mkononi, mistari akilini
coz, life is a battle, battle for survival
kila siku ninahustle, fighting for survival
nazidi kaa ngumu, ata waongeze ushuru
lazima jivunie, haya matunda ya uhuru
na kila kitu kwa maisha, Mola nashukuru. 

CHORUS LYRICS: 
kila siku nina stress, ju mi ninawaza
nashika mic, sauti ninapaza
jana kesho leo, swali moja nauliza
mpaka lini, ah, mpaka lini, ah!

You cannot copy content of this page