Skippa Mistari – Mkenya Daima Lyrics

CHORUS LYRICS:
LAIKKAH & STITCH:
Mimi Mkenya daima, najivunia/ (mi mkenya, mi mkenya) 
sitaki ukabila, yeiyee/ (aa aaaaah, me sitaki/ 
siasa zako sitaki tenaaa/ (sitaki tena, sitaki tena) 
siasa zako sitaki tena (sitaki tena, sitaki tena)………. 

VERSE 1 LYRICS:
BLAZE STITCH:
A thousand ways to die, me nachose kulive/ 
kusurvive kwa hii concrete jungle ni so hard kubelieve/ 
hakuna vita this year/ 
hakuna gunz, hakuna arrows/ 
kama ni stories ya war, basi sitaki kusikia/ 
I stay clear, 
my dear/ 
nakeep a safe distance from, 
totalitarian mind control/ 
am a vegetarian, sina beef kwa soul/ 
u only gain after losing/ 
no sweat no soup in ur bowl/ 
maisha ni fupi kama Jesus wept/ 
the road to happiness, the best secret ever kept/ 
one nation under Jah thou me si Rastafarian/ 
an eye 4 an eye me nasema no/ 
we need more, social amenities n less prisons/ 
more reasons, 
za kubuild the nation/ 
the revolution starts with u/ 
the evolution of a one tongue people/ 
haki kwa wote, popote walipo/ 
wenye mali mafukara, sisi ni wa Kenya… MOJA! 

CHORUS LYRICS: 
Mimi Mkenya daima, najivunia/ (mi mkenya, mi mkenya) 
sitaki ukabila, yeiyee/ (aa aaaaah, me sitaki/ 
siasa zako sitaki tenaaa/ (sitaki tena, sitaki tena) 
siasa zako sitaki tena (sitaki tena, sitaki tena)………. 

VERSE 2 LYRICS:
JUBLAK:
rap kama kawa, 
kichwani bila madawa, 
kitanda bila machawa, 
hawana cha kutugawa, 
kubali ulichopewa, 
kipawa bila mabawa, 
paa kwenye anga Wakenya tuwe wajanja, 
waganga wa kutumanga akili, 
lenga ka malenga siasa za kimalenge, 
undugu kwetu tujenge, 
lahaja isitutenge, 
panga ama jembe, suti ama kitenge/ 
kijana nina nywele kilichobaki tu ni kichana/ 
inaniuma sana wangwana wakipigana/ 
juu ya rangi ya kimwili kwa nini si kujengana/ 
baraka za Maulana kwetu ni ka lawama/ 
I got big dreams, dreams of a star/ 
shining ever bright/ 
see I wanna get far, thats y am holding tight/ 
u see me going places, meeting different faces/ 
i wanna be a force, a source and a course/ 
i wanna wake up with a smile and a queen by my side/ 
thats a good day/ 
a dream of a street, so peaceful and clean/ 
no tension no gun, attention to roses/ 
to see my mama smile/ 
to see my daddy dine/ 
a million bucks from the sales that we make. 

CHORUS LYRICS: 
Mimi Mkenya daima, najivunia/ (mi mkenya, mi mkenya) 
sitaki ukabila, yeiyee/ (aa aaaaah, me sitaki/ 
siasa zako sitaki tenaaa/ (sitaki tena, sitaki tena) 
siasa zako sitaki tena (sitaki tena, sitaki tena)………. 

VERSE 3 LYRICS:
SKIPPA MISTARI:
ndio sikatai, ni wa kabila lako but, 
ata ufe njaa hataleta unga kwako/ 
kabila zote sawa, hakuna ile mbaya/ 
nazidi zichanganya niwe Mkenya halisia/ 
kwa maisha natafuta, kama Mkikuyu/ 
pesa nikipata swagger jo ka Mjaka/ 
shida kwa maisha naziruka ka Maasai/ 
life mbio mbio nakimbia ka Mkale/ 
viongozi hawatupendi, wanapenda kura zetu/ 
baada ya uchaguzi kwetu ni talaka/ 
wanahamia mjini, maisha ya thamani/ 
tunabaki kwenye ghetto, life ya kisoto/ 
kwa nyinyi viongozi, nazidi kutangaza/ 
kushinda uchaguzi ni kwa wingi wa kura/ 
sio mawe na bunduki, mishale na mikuki/ 
mwaka huu nimesema, sitakuwa kibaraka/ 
huku mtaani tukizidi kupigana/ 
viongozi kwa ikulu wanapop champagne na kugawana mamlaka/ 
tunataka peace, yes kura kwa amani/ 
kura kwa amani, the white revolution/ 
daima mi Mkenya, acheni kututenga! 

CHORUS LYRICS: 
Mimi Mkenya daima, najivunia/ (mi mkenya, mi mkenya) 
sitaki ukabila, yeiyee/ (aa aaaaah, me sitaki/ 
siasa zako sitaki tenaaa/ (sitaki tena, sitaki tena) 
siasa zako sitaki tena (sitaki tena, sitaki tena)………. 

OUTRO:
JUBLAK:
Yeah, this a call for the nation. Stitch, Jublak, Skippa Mistari and Laikkah, 
Peace Kenya 
Yo the revolution

You cannot copy content of this page