Labalaa & Wendy – Yuko Juu Lyrics

Verse 1 (Labalaa)
mwendawazim kwenye beat ‘shinda beatnuts
na lazima niwe fit ushike hizi nuts
sura ndim kwenye skizzy nipe beat nasty
kidole tu cha kati kwangu bomboclaat
hii ni yangu tu wakati nikipanda charti
kuipanga mikakati nikipata s’kati
shika ndulo kwenye sura pia trouser na shati
bila kula huwezi fura ukipenda piga bati
ndani ya fura kila skura kile haikosi mitikasi
speedi ni ya sitini kwenye hustle niko kasi
malumbano kwenye hip hop hii ndio movement siwezi acha
magumbano hadi kifo juu I struggle bila wasi
hata kama ni ngum, ni yangu kazi
itabidi unywe sum nikipata zawadi
matatizo ni jukum nikipanda ngazi
kuja unishum juu pete ni almasi
rasta sioni makazi
hustler mi sina tamaa 
sipasi napenda mikasi
staki nikupe nafasi
macho juu kwenye anga, bila jasho siezi manga
kile na-hustle nazichanga
kabla ukweli ione mchanga

Chorus (Wendy)
oooh
Mungu yuko juu
yuko juu

Mungu yuko juu
Mungu yuko juu
yuko juu

Verse 2 (Labalaa)
Kile ninacho huwa ni changu
kile unacho umepata kwangu
bado macho kuona zangu
songa kando wa upande pangu
kile wanataka kumbe ni siku
za malumbano kukatika
hadi struggle kutuliza
hawajachoka kutuliza
wamechoka kutukimbiza
pali imefika huwa si lazma kuzidika
kama ni kusikika huwa ni lazma kuwajibika
hamna kusikitika kabla struggle kukatika
lazma kupatika wakituona tumefika
ni Mombasa nilizaliwa 
hadi jiji nikajaliwa
nala kilichopatiwa
kila mstari umekaliwa
bado sijachoka kuhangaika
sijachoka kumakinika
kijana anapata shika
wasanaa kutatizika
na ikazania, kuzidi kung’ang’ania
ikibidi kupigania
hustle zaidi kabla kuenda Tanzania

Chorus (Wendy)
oooh
Mungu yuko juu
yuko juu

Mungu yuko juu
Mungu yuko juu
yuko juu

Verse 3 (Labalaa)
kila wiki kila day ni survival
kila wiki bila pay mi nadai dough
kila wiki mi na-pray niwe hardcore
si lazima uni-pay, mi na-die for
hii ni struggle niki-fight bila rival
niki-gamble iwe sima ama rifle
ukininyima kesho bima bado nta-hustle
kama nyoka vua ngozi uwe mpya kwenye game
wanapotokwa na machozi wakiwa wapya kwenye fame
wanaponyokwa na kamasi na kukimya
wakikiona hiki kizazi wanakimya
nikimaliza hii verse
waendelee ku-discuss
muendelee kuni-curse
vile huja-feel hii verse
hasira kwenye sura kuwanga vita siezi ngoja
wamenona shinda chura na kuzidi ni uwoga
wanazidi kufa kura kutulisha kila mzoga
wanapenda kunyafura kutunyima pia mboga
hawana sababu ya kutoka wanaandaa bila kutoka
bila sub sijachoka
ni wa-cheap kama bags za mogoka

Chorus (Wendy)
oooh
Mungu yuko juu
yuko juu

Mungu yuko juu
Mungu yuko juu
yuko juu

You cannot copy content of this page