Kakai Kilonzo – Kenya Nchi Yetu Lyrics

huu wimbo ninaimba oh
sio wimbo ni maombi
nikiomba Mwenyezi Mungu oh
aibariki Kenya yangu
kwa jina la Baba na la Mwana oh
Roho Mtakatifu Amina
kwa jina la Baba na la Mwana oh
Roho Mtakatifu Amina
ewe Kenya nchi yangu
ewe Kenya baba yangu
ewe Kenya mama yangu oh
sitakuwacha milele

akili zangu, nguvu zangu oh
nimeziweka mbele yako
bibi yangu na watoto oh
nimewaweka mbele yako
taabu zangu, shida zangu oh
ziangalie Kenya yangu
taabu zangu, shida zangu oh
ziangalie Kenya yangu
ewe Kenya nchi yangu
ewe Kenya baba yangu
ewe Kenya mama yangu oh
sitakuwacha milele

matajiri maskini oh
sisi sote binadamu
matajiri maskini oh
sisi sote binadamu
tusahau majivuno oh
na tuwache kupayuka
tusahau majivuno oh
na tuwache kupayuka
utajiri, majivuno oh
sio tikiti ya mbinguni
utajiri, majivuno oh
sio tikiti ya mbinguni
bahati yako ni ya leo
ile ya kesho ndio yangu
bahati yako ni ya leo
ile ya kesho ndio yangu
ewe Kenya nchi yangu
ewe Kenya baba yangu
ewe Kenya mama yangu oh
sitakuwacha milele

mhalifu twakujua
mharibu twakuona tu
mhalifu twakujua
mharibu twakuona tu
plan zako twazijua
lengo lako twalijua tu
plan zako twazijua
lengo lako twalijua tu
wataka kunyamba Kenya wee
utuharibie hewa
wataka kunyamba Kenya wee
utuharibie hewa
harufu yako twaijua
hata ukipanda ndege
harufu yako twaijua tu
hata ukipanda ndege
ewe Kenya nchi yangu
ewe Kenya baba yangu
ewe Kenya mama yangu oh
sitakuwacha milele

Kenya yangu usijali
ukitukanwa na jirani
Kenya yangu usijali
ukitukanwa na jirani
yeye anaona wivu
kwa vile umeendelea
yeye anaona wivu
kwa vile umeendelea
anakuita nyang’au
amekuita mnyonyaji
anakuita nyang’au
amekuita mnyonyaji
naye azidi kuporomoka
wacha yeye aporomoke
naye azidi kuporomoka
wacha yeye aporomoke
ewe Kenya nchi yangu
ewe Kenya baba yangu
ewe Kenya mama yangu oh
sitakuwacha milele

Kenya wee ni baba yangu
Kenya wee ni baba yangu
Kenya wee ni mama yangu
Kenya wee ni mama yangu
wacha wao waporomoke
wacha wao waporomoke
viongozi wetu tuombeni
viongozi wetu tuombeni
wacha wao waporomoke
wacha wao waporomoke
wananchi tuombeni
wananchi tuombeni
wacha wao waporomoke
wacha wao waporomoke
majeshi yetu kuweni macho
majeshi yetu kuweni macho
wacha wao waporomoke
wacha wao waporomoke…

You cannot copy content of this page