Kachela Kroma feat Burna – Amani tunataka Lyrics

CHORUS LYRICS:
Amani tunataka, Wakenya tuzidi kupendana,
Amani tunataka,Kila sehemu tuwe na umoja,
Amani tunataka, Nchi yetu ya kenya,
Si ya kumwaga damu bure, Umoja wetu ni bora,

VERSE 1 LYRICS:
Si’i wote ni kitu kimoja,
Tusiuwane tupendane,
Mbona tumwage damu kwenye nchi yetu,
Na Kenya ilipata uhuru,
Zamani za kale walitupigania,
Mabeberu tukapata amani kenya,
Na sa’a hivi twapigana si wenyewe,
Viongozi wetu si’i mtupe amani,
Sina baba wala mama,
Mashaka yamenipata ntafanya nini mi mkenya,
Kaka dada washatoweka kama sina haki mie mkenya basi niambieni,
Niwe mturukana wala kikuyu, jaluo, maasai si’i wote ni kitu kimoja,
Japo kabila tofauti mradi si’i wote ni wanakenya,
Tuishi pamoja na amani,

CHORUS LYRICS:
Amani tunataka, Wakenya tuzidi kupendana,
Amani tunataka,Kila sehemu tuwe na umoja,
Amani tunataka, Nchi yetu ya kenya,
Si ya kumwaga damu bure, Umoja wetu ni bora,

VERSE 2 LYRICS:
Cheki, imepofika mi’i nakana nathani imetosha,
Hata Viongozi hawajui ka’a wataikomesha,
Wabuni vyama ambavyo kwetu ni kama picha,
Bila uhakika ya siku haki wataipitisha,
Jioni ikifika kukicha kesho ni patashika,
Baada ya kupata jirani wangu amepigwa shoka,
Nyumba imechmwa na vitu vyote ndani imekwenda,
Ndivyo twajiuliza jee? Ni yupi ametenda,
Maafa hayapunguki Wakenya hawana haki,
Watu wanateseka vibanda wanaviweka,
Vya kuhifadhi watu wetu kama refugees,
Ata baada ya kupata uhuru bado siko free,
Tujiulize, Mbona tuangushane peke’etu bila misingi,
Lo! Na matokeo ni hara ya kwetu kwa wingi,
Inafaamika bila umoja mi’i sikuoni bro,
Bila amani pa kwetu pia sikupi njoo,
Tabua, Penya siasa lazima kuna mikasa,
Chambua, Ni si’i wanainchi twasuffer juu hatuna pesa,
Waendasha gari na kuishi kwa magorofa,
Wakati tunaharibiana na kukimbizana kama panya,

CHORUS LYRICS:
Amani tunataka, Wakenya tuzidi kupendana,
Amani tunataka,Kila sehemu tuwe na umoja,
Amani tunataka, Nchi yetu ya kenya,
Si ya kumwaga damu bure, Umoja wetu ni bora,

VERSE 3 LYRICS:
Amani tunataka si’i mketi viongozi wetu,
Pamoja kwa umoja, mtupe amani mturudishe tuwe pamoja,
Mama tayari ashatoweka, Baba amepigwa panga jana amekufa,
Watoto bado wote wako mashakani, Hawana pahali pa kwenda ni

machungu,
Mama tayari ashatoweka, Baba amepigwa panga jana amekufa,
Watoto bado wote wako mashakani, Hawana pahali pa kwenda ni

machungu,
Nilidhani amani kwetu, Imekita mizizi,
Ila najakushtuka napo jiona mkizi,
Ehh? Kweli nastahili hili, mwachekunyamaza munijibu swali hili,
Mama tayari ashatoweka, Baba amepigwa panga jana amekufa,
Watoto bado wote wako mashakani, Hawana pahali pa kwenda ni

machungu,
Mama tayari ashatoweka, Baba amepigwa panga jana amekufa,
Watoto bado wote wako mashakani, Hawana pahali pa kwenda ni

machungu,Yeyee

CHORUS LYRICS:
Amani tunataka, Wakenya tuzidi kupendana,
Amani tunataka,Kila sehemu tuwe na umoja,
Amani tunataka, Nchi yetu ya kenya,
Si ya kumwaga damu bure, Umoja wetu ni bora

You cannot copy content of this page