Joan Wairimu – Mwanamke Lyrics

Mwanamke hatawaliwi na ngumi,
Mwanamke hatawaliwi na makofi,
anaongozwa kwa kuonyeshwa upendo,
Ukimpenda, atanyenyekea,
Ukimpenda uta muongoza vizuri, bila kungangana kabisa,

(Ukimgonga atakua kichwa ngumu, shauri yako)

Ukimpata mwanaume mzima, yuachukua ngumi kumgonga mke,
Huyu muelewe anayo shida kubwa, yu wahitaji usaidizi,
yu wahitaji usai-idizi, jameni, tene wa haraka, kabisa

(tafuta mwanaume mwenzako mpimane nguvu jamani, mmh)

Sikiliza nikufunulie siri, Sikiliza nikufunulie siri, unacho kihitaji ni kumtunza mkeo,
Ukimtunza naye atakutunza,
Uki muheshimu, naye ata kuheshimu, jameni, bila kungangana kabisa

(aya, ukimpa stress anakurudishia hiyo hiyo tu)

Kazi yake mwanamke nikubeba, una chompa ndicho anachokibeba,
Panda ile mbengu unayotaka kuvuna,
Ukipanda amani, uta ivuna,
Ukipanda upendo, utaivuna,Jamani, raha tele kabisa

(ukimpa kijana, anakupa kijana)
(ukimpa msichana, anakupa Yule Yule msichana)

Ukimpenda, utamuongoza vizuri bila kungangana,
Ukimu heshimu, naye ata kuheshimu, jameni, bila kungangana,
Ukipanda upendo, utauvuna, jameni raha-a tele,
Ukimpenda, utamuongoza vizuri bila kungangana,kabisa!

You cannot copy content of this page