Fundi Konde – Fundi ni Yatima Lyrics

Ninao msiba
fundi ni yatima
kila nikondapo
huwaza mengi
kisa ni cha baba na mama
baba na mama wako ahera

haikuanza sasa
ni kupungukiwa
ndugu zangu wengi kunipoteza
waume kwa wake kuniguru
si amri yangu ni ya mola

walizaliwa kumi
wamoja ni mimi
sita walikwenda
hali ni wadogo
waume watatu na dada zao
tulibaki watatu na wanawake ni wawili

juzi haikutosha
moja alikwenda
sasa tulobaki
hesabu sawa
wa kwanza nami mwisho tu waume
wa kwanza nami wa mwisho tu waume
wa pili kuzaliwa na mdogo we ni wanawake

You cannot copy content of this page