Fadhili Williams – Heshimuni Wazazi Lyrics

wazazi walikulea vizuri
ulipokuwa ungali mdogo
wazazi wako walikupenda
hata wewe ukawapenda sana
walikulea kwa gharama nyingi
wakajinyima na mengi ya dunia
kusudi utakapokuwa
uwe mtu wa maisha mema

sasa umeshateua
umeoa una watoto
mke wako anakuambia
wazazi wako ni wabaya sana

sasa hutaki kuwaona
wazazi wako hata kwa macho
huku mbuki gharama nyingi
walizokulea nazo
kijana toboa wazi
mama na mke ni yupi bora
kama mama hakukulea
hata mke hungelioa

kijana umesahau yote
wazazi waliokufanyia
umeweka bibi mbele
kuliko wazazi wako
ooo hooo
sasa mke wako
anakugombanisha
na wazazi wako
oo hoo
hata anasema
wazazi wako
ni wachafu sana
oo hoo
sitaki kuwaona
hapa nyumbani kwangu
wataleta magonjwa
oo hoo
wee wanyamaza
kimya kama bubu
usije ukawachwa

anayekutukania mama
haki si mtu mwema
kama si mama kukulea
hungeliona dunia ya leo
kijana kumbuka
huwezi kupata
mama mwingine
kote duniani
lakini waweza
kupata mke mwingine
huwezi kupata mama mwingine

You cannot copy content of this page