Eric Wainaina Featuring MC Kah – Fungeni Macho Lyrics
Verse 1
Tulifunga macho kuomba
Tuliibiwa ardhi
Bendera ya Mungu ilipeperuka
Mwafrika akikaa kwa imani
Cheupe kilijiuza
Cheusi kilifukuzwa
Tuliambiwa,˜Imbeni alleluia.
Fungeni macho imbeni.
Chorus
Tumegongwa tumeamka
Tumekanyagwa tumejitoa
Tumelazwa tumesimama heye!
Tumebanwa tumeepuka
Kusulubiwa tumeshuka
Tumeuawa tumefufuka aye!
Verse 2
Mwaka wa 1963
Tulijishindia Uhuru
Bendera ya Mzungu iliteremshwa
Mwafrika alianza kujitawala
Tuliambiwa, ˜Harambee! Harambee!
Furuteni mzigo.
Tuliambiwa Fuata Nyayo!
Fungeni macho fuata Nyayo!
Chorus
Tumegongwa tumeamka
Tumekanyagwa tumejitoa
Tumelazwa tumesimama heye!
Tumebanwa tumeepuka
Kusulubiwa tumeshuka
Tumeuawa tumefufuka aye!
Verse 3
Na bado twangoja wokovu
Twangalia milimani
Twauliza mwokozi ni nani
Twafaa kutazama kiooni
Kila mmoja ni kiongozi
Kila mmoja ni mwalimu
Kila mmoja ni mjenzi
Kila mmoja achukue madaraka