Chuma cha Reli – Nitanunua Helikopter nifugie kuku Lyrics
NITANUNUA HELIKOPTA NIFUGIE KUKU
Kama kwa kuivunja Sheria nitajisikia mtu huru,
Basi pisheni njia jela naja kuishi na sio kuzuru,
Akili imeniambia,
Nachokisema ni muhimu zaidi ya hata navyokisema,
Nisiogope kunena, kwa kuogopa binadamu watasema.
Sio langu lengo kuonyesha umahiri wangu kwenye ushairi,
Nimetumwa niandike chochote nachokipika kwenye akili,
Na ndo maana,
T.V zikipeperusha tuzo za mshairi bora ulimwenguni,
Mi nitakua Sibanduki kwenye kutizama katuni.
Kama kwenye ushairi nitakua sifuati masharti na kanuni,
Basi nafaa nitokee kwenye vitabu vya kumbukumbu kwa ushairi mpya
nilioumbuni
Ni wajibu wangu kujenga kwangu kwa jinsi navyoamini,
Na sio kubomoa kwa mwenzangu eti ndo tukeshe wote gizani.
Utanishtaki vipi nitakapovaa suruali kichwani au tai kiunoni?
Yale yale ya mwanafunzi kumchukia mwalimu anapofeli mtihani.
Ushairi wangu sio majibu ya mtihani wala sishindani
Naandika chochote kinachonitoka kichwani