Chuma cha Reli – Naongea na njaa Lyrics
NAONGEA NA NJAA
Wanasema amerithi Idi Amin ,Kidictator
Hata Masoldier hawaliamini, eti umewateka
Hivi inakufaidi jinsi gani, wana wakiteseka
Tukiumwa umekua kama shatani, we tunacheka
Kwanza ni kweli, umewatuma kina dada wakajiuze?
Umefadhili matapeli, nakuomba hebu nijuze
Bongoflava wanakusingizia, umewalazimisha kuimba mapenzi
Huu upande wa pili pia, bila rap katuni inasemekana huwezi
Mi nmekuchukia, umefanya hadi washkaji kunikimbia
Kitu walichoniambia, kwangu upo sana hawawezi kuvumilia
Si ndo wewe umetuma majambazi, wakapore benki?
Umetupa adhabu ya kazi, na kuabudu centi?
Ila saa njaa,kuna kitu nakushangaa
Hubagui ataaa,kwa misingi ya mtu anapokaa
Natamani kukudis,.ili uniache in peace
Ukienda sitokumiss, unaniuma ile kichiz