Chuma Cha Reli – Nacheka kwenye Misiba Lyrics

Nacheka kwenye misiba
Wote kwa majina yenu,asateni kwa kunifikiria,
Mlichoniambia nimekiskia na nitakizingatia.
Mmeniambia.
Nitembelee mtaalamu wa magonjwa wa akili,
Hilo la kwanza halafu na la pili,
Nachokifanya nikikifanya nifanye japo kwa siri,
Unaona unafiki wenu ulivyokithiri?
Samahani nitawavunja moyo kwa kutotembelea mtaalamu,
Na nikimpitia sema ni ile tu kumpa salamu.
Nitawaambia tupo east Africa na sio armsterdam,
Ili kuthibitishia jinsi gani navyojifahamu,
Yaani, nimekuja na ile akili yangu timamu.
Mida na misiba ya kulia ikitimia nitalia
Ila sio kwenye hii misiba ya kujitakia.
Hamna aliyepoteza msibani kama marehemu japo ametulia
Na wasioathirika sana wanajilazimisha kulia
Hamjui wapo wanovunja sheria kwa kuwa
Kitakachofatia wapo tayari kukigharamia?
Niacheni basi mimi kicheko niangue,
Kutakavyokua na kuwe.
Maana daktari alisema kituflani kuhusu kucheka.
Eti kuwa maisha yangu yataongezeka
Sijali mtanichukia wote mnaoongwa bila kusikia
Na kiburi mnachojitia kwa mafanikio madogo tu mliyoyafikia
Kitakachofuatia,
Ni misiba ya kujitakia.
Nitoeni kwenye orodha ya watu watakaolia msibani

You cannot copy content of this page