Chuma Cha Reli – Mi si Gynaecologist Lyrics

MI SI GYNAECOLOGIST
Mna bahati mmekua na sio tena watoto.
Kinyume na hivyo, ningewafuata popote mlipo.
Mkononi na kiboko.
Kazi ya kuwafunza watu wazima adabu.
Sitaki kusema imenishinda, lakini imenipa taabu.
Mlinishauri Mbwa  wangu akifa nijifanye hainihusu.
Nipigieni makofi sababu mlilonituma nimelijaribu
Tatizo, ule mzoga umenichafulia hewa pale pangu. 
Kila siku nabana pua, nimebadili umbile alilonipa Mungu.
Ukimwona anaenda kuogelea amevalia Suti na tai,
Kama sio filamu anaigiza mwelekeze  kua haifai.
Nitawaonya dhidi ya kula kabla ya kujua pa kujisaidia.
Eti mnakula kwa macho tu, ambayo hayana pazia?
Ndio hayana pazia lakini si  unachagua pa kuangalia?
Vingi vilivyo dukani (kama sio vyote) vinauzwa.
Na ukifanana na kahaba, ndivyo utakavyoitwa.
Niliuliza maana ya neno fashion na ilinjibu kamusi
Na si ajabu sikuona popote mlipoambiwa mtembee uchi.
Na ule msemo wenu wa kujaribu kuyamiza malalamishi,
Eti mind your busness sisi tunaenda na wakati.
Kweli?
Hamwogopi mnafanya mwanamke aonekane kama kifaa?
Kwa jinsi mnavyovaa?
Nitakuheshimu na kukuoa ukinionyesha una akili,
Na sio ukinifumbulia mwili.
Vaa nguo mi sio gynaecologist.

You cannot copy content of this page