Chuma Cha Reli – Baiskeli ya wanawake Lyrics

INTRO:
CCR…audio kusini. Yeah hawa Madem ni
gonjwa amatumiwa au?Yeah skia mmmm

VERSE 1 LYRICS:
Ni kijana mtanashati tena mwenye bahati
Kila siku kwenye party anawalenga kwa manoti
Manicure, pedicure anajizijua
Kwenye jua kwenye mvua atazingua
Anaishi kisharobaro shingoni na ming’aro
Kila siku kwa mitaro hataki shika haro
Kula hepi kula bata eti kwake ndo mitindo
Hataki mi narap, eti tukale mizigo
Nkama vile huyu jamaa kiakili hajakomaa
Anawapa rubudani kisha anaachwa kwenye mataa
Nshajaribu kumweleza, ila akaniita pweza
Anakula kwa mkupuo, kama dunia inakwisha
Madukani ana madeni mfukoni hana mapeni
Akipita anatumia kisha anabisha niacheni
Kama jana ana rehema, leo ashamtema
Anawamega kwa foleni mwanzo mwisho kisha tena.

Chorus x 2

VERSE 2 LYRICS:
Mi nona bora nimwache aishi maisha yake
Afunzwe na dunia kama sio yule mamake
Ila sasa mi ni gangsta tena mi ni rasta
Namjali kichizi, sitaki aishi kihustler
Ona anavyomegwa kama dume halina maana
Ona anavyomegwa na watoto wadogo sana
Ona anavyomegwa na madem wa kila aina
Ona anavyochezwa ngo…………..ma
Anaamini ana talanta kwa jinsi wanavyodata
Madem anawapata kila anaemtaka
Wanamwona kama benki yaani buzi la micenti
Akishalewa mapenzi wanamwacha bila cash(i)
Wanamwendesha kwa kasi bila hata ya makini
Kama gari la jambazi wanamwacha mashakani x2

Chorus

VERSE 3 LYRICS:
Mchizi naomba unishikie huko uliko uturudie
Madem wasikutumie tunakumiss sie
Hadithi ya maisha yako eastfrica nshawapea
Najua utakasirika utniita hata mmbeya
Kama jinsi ulivyoskia basi mi ndo nakwambia
Bora tu ungekimbia madem usiwachumbia
Mi nona bora ukawekeze uachane na vicheche
Wanasubiri ufilisike ili waje wakuache
Najua utaniambia its non of ma business
Lakini nahofia its kind of a sickness
Mchizi amasha akili madem wanakutapeli
Unadhani uko kwa reli kumbe ushafeli
Mchizi naomba uniskie huko uliko uturudie
Madem wasikutumie tunakumiss sie
Hadithi ya maisha yako eastfrica nshawapea
Najua utakasirika utaniita hata mmbeya

Chorus x 4

OUTRO:     
Nenda ukamwambie kama sio ana act movie
Basi aache kuongeza maisha chumvi
A.K Audio Kusini.

You cannot copy content of this page