Rose Muhando – Sitanyamaza Lyrics

Eeeehhhh…. Mimi Mungu (Me, God)
Matendo nitalia, Kwa sinani nitaomboleza
Sodoma nitanung’unika, Mipakani nitashambulia
Mijini wameniacha,Kila mara nitashambulia
Maisha ya wanadamu, Yamenichosha….

Oh oh mimi
Sitanyamaza, wala sitanyamaza
Lakini nitalipa ujira wa vifuani mwao
Maovu yenu ninyi, pamoja na baba zenu
nasema nitalipa ndio mjue mimi ni Bwana
Mmefukiza uvumba, na kunitukana
Kwa ajili ya haya mtajutia vitani mwenu?(repeat)

mmefanya uzinzi katikati ya milima
Usiku wa manane mmefanya ukahaba
Kwenye njia kuu na vichochoro mmefanya mapatano
Kwenye mialoni na mipera mmefanya machukizo (repeat)

Ulitumaini uzuri wako ukafanya ukahaba
Kila kijana aliyepita ulimwona anafaa
Awe mzuri na sura mbaya ulifunua marinda

Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda
Wako wapi mapenzi zako mbona sasa unakonda
Wako wapi wapenzi wako mbona sasa unakonda
Wako wapi waelizamu (?) wako mbona sasa unakonda

Miji mizuri imekuwa ukiwa
Majumba mazuri yamefungwa kabisa
Wana wa wana wamebaki yatima
Kiburi chamuwamu(?) imekoma kabisa (repeat)

Hebu sasa piga kelele uliye kahaba,
Shika kinubi omboleza upate kukumbukwa (repeat)

Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye
Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye (repeat)

Lakini Bwana asema hivi, nitawaponya
Yeye mwenyewe aahidi, nitawabariki
Mimi ni alfa na omega, mwanzo na mwisho
Jamani mimi ni mungu, mwingine hapana

Nirudieni mimi niwasamehe, Nasema mgeukeni sasa niwaponye (repeat)

You cannot copy content of this page