Meg C & Bamboo – Nipe Lyrics

Verse 1
sikiza,
nimetosheka na uwongo
hunielezi unakotoka
hufahamu thamani ya kitu
paka kikitoweka
nakuomba njoo kwa mara mwisho
nikuone sitakupa jukumu
navyohitaji kuwa nawe
niwe na wewe leo tu

Chorus
nipe
usiku moja nawe
hivyo ndivyo nataka
nataka nikushike
usiku moja
usiku moja nawe
hivyo ndivyo nakuhisi
hata na wewe pia

Verse 2
na sasa,
waniambia bado wanipenda
huku umeniacha niende
nasikitika bidii yako imechelewa
penzi limekwisha
haina haja ya kungoja
naenda nikufahamishe
ninavyohitaji kuwa nawe
niwe na wewe leo tu

Chorus
nipe
usiku moja nawe
hivyo ndivyo nataka
nataka nikushike
usiku moja
usiku moja nawe
hivyo ndivyo nakuhisi
hata na wewe pia

Verse 3 (Bamboo)
yo Meg C kwa muda sijakuona
ni miaka tatu na sasa nashindwa mbona
kazi yako ya kunitibu umeshagoma
noma, kweli uliendanga kusoma
nime-miss siku zetu za beer na nyama choma
kweli nimekukosa naona bado wang’aa
siku moja ingine ni sawa inatufaa
Bamboo and you
(Meg C)
naomba niwe nawe
japo siku moja
tafadhali
usitake zaidi
kwa kweli hatuwezi rudiana
machungu niliohisi
siwezi kuyasahau
usikumbuke usuhuba
sahau yalopita
kwani hayo ni ya kale
nipe usiku moja nawe

Chorus
nipe
usiku moja nawe
hivyo ndivyo nataka
nataka nikushike
usiku moja
usiku moja nawe
hivyo ndivyo nakuhisi
hata na wewe pia

You cannot copy content of this page