Maleek, Jua Cali, Nonini & Talia – Nawaza Lyrics

Intro
Oya oya
Jua
Maleek
Nonini
Sidney City kwenye studio
Collabo
Jua twende kazi

Verse 1 (Jua Cali)
Nikon a siri mingi sijui leo niwaambie,
Sijui leo niwaskizie
Tembea na ID beshte ama utashikwa, 
Club majuu beshte utakaziwa kuingia
Ni saa nane nimeusi taxi mi nakutupa,
Ni giza hata hauwezi ona through hiyo dirisha
Najua si poa lakini nimenoki sista ya beshte yangu,
Sijui itakuwaje
Nataka kufungua studio na sina ganji, 
Mi huingiza baridi kabla niingie stage
Naota vitu mbaya ka niko gauge, 
Ma faceoff ma faceoff ka Nicholas Cage
Niamshe saa mbili twende ile shuguli, Nikikosa ile noti ntanoki
Umeficha wapi ile kitu nitolee nivute,
Mi ni striker kwa ile kitu mtu wangu kanoute
Niongezee nguve ndom ndio nishute

Chorus (Talia)
Nawaza, Maisha yangu,
Itakuwaje bila wewe siri zangu ntamwambia nani
Mi nawaza ebu niambie mbona wewe kaenda mbali rafiki yangu,
Ndugu yangu lala polepole

Verse 2 (Nonini)
Beshte yangu alisema haekangi maadui upande ya kushoto
Yuweka kulia ndio anakaribia
Mtoto wangu juzi akaniambia hataki kupata motto
Ataenda Uni ah saa hii ametulia
Baba yangu akaniambia usiwahi argue na father
Utakaa ka yeye usipige makelele 
Cousin yangu akaniambia nenda shule jo usome bwana
Nikamwambia Makerere flight manze si bwerere 
Maparo wanadai Nonini jo anaimba ngoma chafu
Advice jamii wachana na msanii 
Sista akaniambia weka God kwanza alafu omba kanisani
Pia njiani mathangu akaniambia ananipenda vile chupa hupenda bar tester
Dunda kesha nyumba ntajenga
Bratha akaniacha lakini bado yuko kwa roho
Kila December ntam-remember ocha kwa grave mana tu ntaweka
Ma-playa hater wakadai industry sitatoboa 
Niko bado ka cartoons za Gado
Utaniskia mpaka majani ya maua ije ufikirie rangi ya manjano 
Kumaanisha siendi popote
Kokote sosote mi ni wireless bado na-rule industry ka Milton Obote
Sa mzeya wangu Maleek mzeya niokote

Chorus (Talia)
Nawaza, Maisha yangu, 
Itakuwaje bila wewe siri zangu ntamwambia nani
Mi nawaza ebu niambie mbona wewe kaenda mbali rafiki yangu, 
ndugu yangu lala polepole

Verse 3 (Maleek)
Siku mingi mi hukaa,
siku mingi mi huwaza, 
siku mingi ni fikira
Hali ya kusikitika ni vile sitafika kutajirika ufukara inanikaba
Album ntaangusha lakini hela sitapata
Ni show kila mara, 
Mamanzi wananitaka lakini mapromoter wananikazia
Wananifungia hazia 
Pengine nikishikana na Nonini na Jua hawa madame watanijua
Lakini mpaka hapo biashara niko hustle Sidney mpaka Calif
Hizi ngoma zinazosalifu
Genge inashikana na hip-hop, hii basi 
Ni ya mashabiki hii ni ya kila mtaa Nairobi mpaka Dar
Nawaza ukiniskia bro ka utajazwa na furaha 
Juu bro wako mkiddy siku hizi anang’aa
Na tracki zake zote kwa ma-charti zinapaa, nimekuwa star kwa mtaa
Lakini haki ya nani hiyo sifa nimekataa 
Hainifai hata, hiyo ni sifa yako Karani
Hiyo ni sifa ulipewa mtaani, hainifai jamani, nimewaza nimewazua
Wazuri hufa wachanga ni jambo nimegundua 
Na malaika wake basi Mola amechukua
Carol night forever ni album jo ni poa 
Lazima watakubali lazima watakujua

Chorus (Talia)
Nawaza, Maisha yangu,
Itakuwaje bila wewe siri zangu ntamwambia nani
Mi nawaza ebu niambie mbona wewe kaenda mbali rafiki yangu,
Ndugu yangu lala polepole

You cannot copy content of this page