Les Wanyika – Ombi Lako Lyrics

Swali lako mwana mama nakujibu leo
kuwa siwezi oh, siwezi oh, mama

mimi nilielewa tokea zamani
jasho lakutoka ukiniona na yule

eeh Noni nakupenda si ajabu kwa mimi
kwani imekuwa ni wimbo duniani

nakusihi na mama samahani oh
nilijua wa ziwa ni hadaa
zile ni hadithi kwangu ulisimulia
kwani sioni dalili za ukweli wako eeh

ombi lako ulifoli na mimi oh
nimwache wangu nimpendaye
nia na kusudi lako ni kutuvuruga
wengi walishindwa mi nitakuweza wapi oh

ombi lako ulifoli na mimi oh
nimwache wangu nimpendaye
nia na kusudi lako ni kutuvuruga
wengi walishindwa mi nitakuweza wapi oh

mama samahani oh
tena uniache
kwani nafahamu utakuja  nijutisha eeh

wengi walijuta kuwapoteza wapenzi
juu ya kudanganywa hivyo mimi naepuka eeh
kwanza jiulize
ili ujielezee
tatu ujijibu ombi lako mwana mama eeh
hiyo ni aibu
tena ni fedheha
kwani ule wangu wewe ni shangazi yako eeh

mama samahani oh
tena uniache
kwani nafahamu utakuja  nijutisha eeh

wengi walijuta kuwapoteza wapenzi
juu ya kudanganywa hivyo mimi naepuka eeh

You cannot copy content of this page