Kilio – Ten marks Lyrics

VERSE 1 LYRICS:
Nina bars kama jela so,nikipepea unahema,ninacho
chakupepeta hewa,nikipuliza hutaweza bro,kwenye mishipa
ninapita ninayo ya kukutisha,nisha,gonga milango kwenye
beat ya commando,nikispit unaswallow,kwenye street
rapper songa kando,inamaana wangu mama kanifunza ni
si,poteze ndama kwenye shamba kwani mi mzazi,kwenye
sanaa,wasanii hawana saa,hawashiki hii fasihi wanahisi
hii chapaa,nina,mabawa kwenye bega na kahawa kwenye
meza,ukicheza utaweza kuimeza?,ni mafumbo kwa mziki na
midundo,wacha fujo,vipi dada tingiza chako kiuno,you
know,jina kilio vyangu vina simulio,hili ndilo hip hop
kaulizwa sema ndio,piga picha kuonyesha anayepita kwenye
njia,nikiita waitika,nikipita wanapisha,nadhani
shakupatia,siri inayo zidi akili mithili ya madini
kwenye mwili ya msudi, kwa maksudi, na ninarudi*

Jaza
mistari kisha pata ten marks. Ten marks sio funny kwa
hii fani tafadhali.

CHORUS (Beats playing)

VERSE 2 LYRICS:
Ninalia nikiskia,marraper wanatia,mistari bila plani
hawajali zingatia vina,16 ama 32 bars kwenye
verse,discuss,na award ten marks,rapper wacha ubishi
pisha works,haijalishi mavaz ama class,utumishi kwa
mafans,ni a must,kichwa kutudunda,kucha kuturunda,ziki
vuna rumba,mziki huu ni mzuka, uh, hebu jiunge
nasi,upate jua wazi,mziki ni mzizi wa Africa tandu
jadi,kupita almasi kwenye chati, oh Lord have
mercy,hawajui ni wakati,vunjika kwenye mifupa
utadhani,umegongwa na gari ni ajali samahani uniwie
radhi, ni vile nimejaza fani kwa mistari kuhifadhi
nikidhani uta-burry akili ndani,mziki hizi siku hizi
zinatungwa hivi hivi sizihisi sikioni siziskizi,wataka
imba kama Weezy, huo ni uwizi, suruali cha kuomba
hakisitiri, uko fake kama suti sato, ama kama chama cha
mafago, shika kichana utahama usipochanuka, tukikutana
we tazama umetambuka, nakuja hivi, ndio masela na
machizi wajibambe nizijaze zao cd, niifanye kwao eazy,
kunicheki kwenye tv sio siri Kili nilishawasili

CHORUS (Beats playing)

VERSE 3 LYRICS:
So nago on, kuleta show, ukidrop uta-mop hii floor, ju
janitor ameshindwa shika flow, nazika chini low,
ukirusha punch line nathrow blows, ukija hivi itakubidi
umepunguza speedy, ukipuuza utajikuta na ma-looser
chini, hip hop hili, kwangu mimi dini, basi easy
kumetameta kama madini. Skiza hii, kutoka Kilio.

You cannot copy content of this page