Kilio – Marashi ya jasho Lyrics

VERSE 1 LYRICS:
Tuko kwenye mbio kama Michelin, skio keen listening,
jicho still visioning, past the ceiling ju hii mission
ni, possibility kusonga, milango gonga, jifungulie
boarder, sky ni limit no more na-fight kuzidi war so,
why ni-limit hii flow close show, visanga toka slavery
huwanga vina measure hii, nguvu za wasela kuweza
remember ni, jasho letu kumwagika siku kutupita
tukinung’unika, hivi lini tutashika, mawaidha, toka babu
zetu zile maidha, kawaida, kuchafuka ukitafuta mayai na,
usipolima shamba, basi kijana, dunia kulilia fikiria
wako mama, na-set off, yangu journey niki-step on, jasho
kwenye barabara Inshaallah nta-take off.

CHORUS:
Beats playing

VERSE 2 LYRICS:
Na basi mi, nitailisha yangu family, haijalishi jinsi
bora dishi mezani, inabidi, kutia ndani sana yangu
bidii, ndipo nili, ingia kwa hii sanaa ya mziki, na sa,
natazama vijana wengi mitaa, kujaza mavibanda kuwaza
wakizubaa, inakaa, ni kama wanangoja pata mboga wanaomba
wetu Mola njaa kufanya kuokoka, ona, kina nani,
wana-lazy kwenye teli bila money, madeni ju ulevi
kutamani, imani yao wameweka kwenye sugar mummy mitaani,
ili kudishi yao mali, jamani.

Yenyewe najua ni ngumu. Kutafuta ni noma, jua bado
itachoma. Lakini fungua macho utaona. Jua ukishuka
utapona, jasho ni marashi ya bidii utaona?

CHORUS:
Beats playing

VERSE 3 LYRICS:
So nina mic moja, mistari kama mia, mashida kupitia
kisha studio naingia, nawaimbia leo skia, kesho
nawauzia, shida zangu hamsini kuzaa shilingi mia, naye
bibi atazaa, nitaitwa baba ni furaha, nitajikaza kwani
mi shujaa, ina maana nitamanga, ju jasho ninamwaga jingi
sana, baraka ninapanda kwenye shamba, Inshaallah!

Utaishi vipi bila ku-try, kufanya kazi, utawa jambazi,
kisha u-cry ukila nyasi, na si, kazi ya wazazi
kuku-feed, hizi streets watoto wadogo this wana-feel.
Wacha upuzi weh, jipe ujuzi eeh.

You cannot copy content of this page