Kilio – Genesis Lyrics

VERSE 1 LYRICS:
Tunastrugle, kwa milango na bado, kwenye njia tuko
kando, trouble ku-handle, tribal ni backbone ya politics
still ni more tricks, hadi politrix ni convincing of a
better future lakini bado missing kwenye streets, maisha
ya jamii iko chini umaskini utazidi hadi lini?

CHORUS LYRICS:
Karibu Genesis
Hii ni mwanzo mambo bao
mzizi toka ng’ambo

VERSE 2 LYRICS:
Tembea nami, don’t be lonely juu ya ukoloni ya walami,
hawako sorry kwani huoni hawana-worry nasi
tuko-mourning, toka jioni hadi morning, tukiwaza wetu
babu na nyanya, kwenye shamba, wakilima nyanya,
wakijikaza, kuwalisha mamba, inaniuma sana ni kama,
nilikuwa nao wakifungwa kamba, kusahau ni dharau,
makarau ndio hao bado wanacheza vinanda, za kututenga,
medali kwa bega, wanabeba, vijana kwenye jela, ju ya
hatia, zisizokaribia, mila zetu za Africa tabia,
kunatisha, tumepita metre kufika hili stage la kuita,
vita miongoni mwetu kisha, kuwaalika kutizama shida,
tukiwapisha waje kutuita, wajinga, siwalaumu kwani sumu
ndugu anampa ndugu anywe kudhuru, hii ni nini, hamna
siri ya mtu mbili tangu lini tugeuzwe akili, tunaishi na
majini inabidi, usaliti tugeuze iwe dini, ni uongo tu,
inua mikono juu, bila sisi hawangejenga hizi, buildings,
ona pyramid za Egypt, civilization hawaku-mention
ilitoka toka hili nation.

CHORUS LYRICS:
Karibu Genesis
Hii ni mwanzo mambo bao
mzizi toka ng’ambo

VERSE 3 LYRICS:
Race for supremacy, wali-create, toka hate, yao ya
ma-race, kutu-make inferior, juu ya ngozi ambayo ina,
fanana na ina, mpaka wakapinda, images, kwenye zetu
brain, ili tubaki savages, tizama sasa mpaka wasichana
weusi wanazidi ngangana, kufanana kama wazungu, kichwani
weave, licha ya uchungu, na wavulana wakiona kwamba,
hawa wasichana sio warembo kama, wale wale ambao wana,
jaribu kufwata kama kondoo, kutamani more, hadi
ku-bleach uso, because, tuna-feel tuko below so, in the
process tuna-posses inferiority complex, tukihisi
content, marraper kutumiwa kama ma-puppet, kurudisha
chini ladhaa ya cassette, kama nasset wananyoa yetu utu
wa culture waki-perfect, the little ways, to decay the
black mind to trash so fast everyday, okay, tuna-feel
it, toka shule ya msingi, wakitulimit, space ya
kufikiri, black ina-evolve, tuko so slow, inashow so
unity tuinvolve, kwenye motion, tuna lose, tuki-choose,
kuwa used, na ma-umbu tukilenga uchungu, usiwe stupid,
ukiziba uchi utazaa vipi we mpuzi?

You cannot copy content of this page