K-South – Tunapenda Zote Lyrics

Verse 1 (Bamboo)
huwezi niona siku hizi niko busy
kichizi kazi mara tizi
K-South umebadilisha style siku hizi
pengine wengine bana sio sisi
napiga simu sana ndani ya ofisi
lakini vichwa hazijaiva bado mbichi
nakuambia ukweli jo mi sikufichi
bado sijapata ndai mimi
natafuta juu natafuta chini
mara polisi wamekamata mimi
jo nashindwa bana nimefanya nini
apana kuna kitu mnataka nyinyi
ndio maana mnafuatafuata mimi
kuskia hiyo afande akasema hivi…
kuskia hiyo afande akasema hivi

Chorus
tunapenda zote
nyama ya ng’ombe
ugali, kachumbari ili watu wasikonde

tunapenda zote
nyama ya ng’ombe
ugali, kachumbari ili watu wasikonde

Verse 2 (Jerry Doobiez)

hii kuwaka bila ku-dish mi nimekoma
leo home hakuna dishi juu mboch amegoma
si basi ntapitia tu kawaida for nyama choma
si unaona siku hizi Doobiez huwanga amenona
sa mbona nikonde kuna mali mi naponda
waiter, number
mbili mbili baridi kabla hiyo kilo ya steaki na marafiki
kata kachumbari na nyanya za marikiti
mishkaki fiti hadi nasanya vijiti
ma-toothpick hawana mi nina vibiriti
kwenda choo nijisaidie hakuna T.P
kurudi nakuta nimeshanyang’anywa kiti
nipe risiti nilipe jo mi nijikate
kuna party nimealikwa staki nihate
jo kuna mamanzi keroro na manyake
manyake babake maanake…he-ya

Chorus
tunapenda zote
nyama ya ng’ombe
ugali, kachumbari ili watu wasikonde

tunapenda zote
nyama ya ng’ombe
ugali, kachumbari ili watu wasikonde

Verse 3 (Jerry Doobiez)
nimeskuma wiki nzima na mboga sima
sa kubadilisha lazima watu kushiba
mashida nyumbani giza na nikazima stima
wanasema rap si mziki ni pararira
kwangu wera ni wera bana bora hela
ya keroro na kerea
na mkiropokwa home ntaendelea
kusota ntatoroka kupora hadi kuzorota
na nikikosa za mboga eh, ntakinda mbota
oka, oka, oka naki
(Bamboo)
bizzy bizzy blaze blaze blazo
jo tuki-blow
nunua ka soo
bizzy bizzy blaze blaze blaze
nilizaliwa MC uliza mathee
usiniambie hunikumbuki ama hunijui
na mi nilikuambia
mi huwanga ni mrui
naroga watu kama wakamba kule kitui
akina Kalonzo Musyoka musyoki
watu wananoki na jo sichoki
toka mbio kama hockey stick za Njoki
kama wakubali sema okey dokey
napenda nyama choma na kachumbari
kama kilo moja na kiugali
hii ni ya wakenya wa kila mahali

Chorus
tunapenda zote
nyama ya ng’ombe
ugali, kachumbari ili watu wasikonde

tunapenda zote
nyama ya ng’ombe
ugali, kachumbari ili watu wasikonde…

tunapenda tembo
wasichana warembo
minazi na bahari 
kwenda pole ndio mwendo

tunapenda tembo
wasichana warembo
minazi na bahari 
kwenda pole ndio mwendo

You cannot copy content of this page