Jua Cali – Nakuroga Lyrics

Intro
Ngoma mpya
Calif records
Ka kawaida simnajua hii ni genge
Eeeh!
Juacali
Unaniroga
Tunawaroga
Twende twende kazi 

Verse 1
Nimekua nakuona kutoka kitambo 
Daily niko ngazini nakula moto na hii mwili yako
Nilikua nashindwa ntaongea aje na wewe
Lakini leo jo sina ujanja sababu nakutaka wewe
Unaitwa aje eeeh! hio ni jina poa 
Mi ni Jua Cali na ngoma zangu ni poa 
Calif Records ushaniskia kwa radio
Nishaona mamanzi wengi sana au sio?
Lakini we ndio wa kwanza jo kupeleka damu yangu mbio
We ni kitu kushinda mamanzi wote wa Nairobi
Lips wazimu mapua imechongwa unakaa poa na hio marvin ukiskiza walkie
Naona unaskia baridi wacha nikupe jacko yangu uvae
Usiogope ikona joto sana we ivae
Leta hio bag yako nikusaidie kubeba
Utapita hapa siku gani ningependa kukuona tena
Saa wacha tutembee pamoja tukiongea
Usiogope wale jamaa wanatuangalia me nshawazoea
Nikivuta vidole zangu hivi ona wakipotea

Chorus
Nakuroga
Unaniroga
Heeey heeey
Tufanye nini?
turogane

nakuroga
Unaniroga
Heeey
Tufanye nini?
turogane

Verse 2
Una smile poa kuna mtu ashakuambia
Una dimples poa kuna mtu ashakuambia
Wacha basi nikue mtu wa kwanza kukuambia hivyo
Ukipita njiani hizo vitu zako zitafanya watu wengi wavunje shingo
Ukicheka hivyo najua kitu iko
Naeza shika nywele zako kidogo?
Oooh jo! 
Kusema tu ukweli hizo nguo umevaa zinakutoa poa
Staki kukuchekesha sana mpaka uanze kukohoa
Ona vile mwili yako imejichonga
Kichwa yako inakuuma wacha nikuu__ utapona
Unaniambia ati chali yako alikutia zii
Vile uko sawa mi sioni ka ntakuacha
Uamini usiamini vile niko hivi
Sijakua na manzi for three years hivi
Saa hii najua unafikiria huyu jamaa anakudanganya
Si nishamwona mara nyingi mtaani akihanya
Labda uliona mtu mwengine si mimi
Mi nataka tu kukuroga kwani iko nini!
Aaah! Tushafika hapa ndio kwenu
Pia me naishi pale si mbali kwa ile nyumba jo 
Ikona fence ya… fence ya…

Chorus
Nakuroga
Unaniroga
Heeey heeey
Tufanye nini?
turogane

nakuroga
Unaniroga
Heeey
Tufanye nini?
turogane

Verse 3
Saa hii ni four months na si bado ni ma beste
Kuna machali hawataki kutuona pamoja itabidi nimewapiga mateke
Mathako naye nimeona aah hana noma sana
Mbuyu wako nilimwona jana mara ya kwanza
Vile aliniangalia jo najua anaeza nichapa mbaya
Lakini sahau hio sai hii ni time yetu me na wewe
Ka we ni manzi mapombe tuende bar ulewe
Ka we ni manzi maklabu tuende ngoma ucheze
Ka we ni manzi majuo tuende kwa popo upewe
Ni tamu ukikunywa mingi sana usitete
Naona sai uko sawa umeshibashiba
Tuna-relax kwa bench unaongea na mi nakushikashika
Hatuezi enda home sa hii kuna rationing
Sa hii ni saa sita najua hao mafala wamezima stima
Time mingi nikona wewe mpaka mabeste wanazusha
Siku hizi Jua Cali amejipoteza inaonekana ametutupa
Hawajui nsipokuona naeza kuwa mgonjwa
Nimekunoki hiyo design mpaka nashikwa na ugonjwa
A la! Nataka kukuroga we ndio unaniroga
ebu ngoja
leo umeng’ara kwani tunaenda wapi?
Ooooh! Ile movie nilikua nimesahau eeh! inaanza saa ngapi
Eeeh! inaanza saa ngapi?

Chorus
Nakuroga
Unaniroga
Heeey heeey
Tufanye nini?
turogane

nakuroga
Unaniroga
Heeey
Tufanye nini?
turogane

You cannot copy content of this page