Jua Cali – Miaka Lyrics

Miaka moja…
na-breathe hewa yangu ya kwanza nimezaliwa
miaka mbili…
meno zinanitoka chakula nateremsha na maziwa
miaka tatu…
niko poa kutembea mathee leo tunaenda wapi?
miaka nne…
nimeanza kujuana na watoi wengine age yangu hapa mtaani
miaka tano…
napelekwa nursery nalia mathee usiniache hapa, usiniache hapa
miaka sita…
najikuta kwa fight yangu ya kwanza lakini huu mkiddy ananichapa
miaka saba…
naingia primo kwenye uniform naskia raha
miaka nane…
nishajua kuandika nipe biro ni vile si hufanya
miaka tisa…
nachimba mguu yangu vibaya nikicheza ball mguu tupu
miaka kumi…
natulia kejani wiki tatu mwanaume nipe supu

miaka kumi moja…
naanza kuenda roundi za dush na za mbaa
miaka kumi mbili…
napeleka beta high speed inanibamba
miaka kumi tatu…
diwali inafika lipua watu na baruti
miaka kumi nne…
haiya nini hizi zinamea karibu na mkuki?
miaka kumi tano…
mono lakini siku ya kwanza tuna-skive chuo
miaka kumi sita…
jioni jam session na hizo nguo
miaka kumi saba…
ndoto za maji zinanisumbua
miaka kumi nane…
chuo kwisha mtu mzima ID nachukua
miaka kumi tisa…
mkulima napalilia kwa mara ya kwanza
miaka kumi kumi…
naingia kejani natoa noma huku niki-stagger

miaka mbili moja…
naingia industry natoa ngoma yangu ya kwanza
miaka mbili mbili…
eh, kumbe show huwa ngumu hivi kupata
miaka mbili tatu…
naingia colle si kuna watoto huku
miaka mbili nne…
sina fare, sina lunch maisha ngumu
miaka mbili tano…
wacha niende inda nione ka ntaangukia
miaka mbili sita…
eh hamsini jioni Mumbi si unaniumiza
miaka mbili saba…
haidhuru mtu wenu wa nguvu anatia bidii
miaka mbili nane…
champagne wapi naenda MTV!
miaka hamsini…
niko club nazitoka
miaka soo…
viagra bado naziokota

You cannot copy content of this page