Jua Cali & K-Soja – Mabeste Damu Lyrics

Verse 1 (K-Soja)
Beste tuko pamoja tangu siku za kusota
ma-shorty kibao tuliwachota, siwezi sahau
nakumbuka ukipata forty tunaikula mbao mbao
unakumbuka ule mama ulicheki ule buda asikuwai kuseti kwa makarao
wee ni mtu wangu kama ndugu
siwezi kurushia mkono hata hii life ikiwa sugu
usiwai skia story za hawa mafala najua vile inatubamba wanaskilia machungu
ebu kwanza gonga glass wajue vile hapa damu ni nzito kuliko maji
tutazidi kuwa pamoja hivi hata kama hatuna ganji
tutazidi kupepea na hii life bila wasi wasi
mtaa yako ni yangu
shida zako ni zangu
‘tazidi kuwa hivi mabeste… damu
hata ka ulidandiwangwa jamu anajua haikuwa noma yako
hawa mafala walikuseti lakini unajua mi ntazidi kuchungia familia yako
mtoi wako ni msoo saa hii anakaa tu kama wewe
najua huko ni kuzii beste chunga nyuma wasikufungie ka buti ya gari
utatoka soon tutaendelea na hii maisha yetu usijali
hata kesho asubuhi ntapitia nikuletee tu mkate na mangale

Verse 2 (Jua Cali)
eh, chali yangu
unacheka hii kipara yangu nini?
kesho ni public holiday naskia tutapikiwa maini
au sio?
mi nashukuru kila kitu umenifanyia
mi huku ndani kimwanaume navumilia
niliariwa juzi lakini leo niko mzima
lunch nimekula na sijawai shiba… hivi
kwa nini tuki-hustle mtaani bado si huitwa waizi
tumbo ni ndogo na daily inaitisha
kumbo ni ndogo na daily inaumiza
kachawa za hapa ndani ni noma
make sure ukuwe umeniletea sabuni ya kuoga
jioni saa kumi najianika kwa jua
baadaye cell tunaosha na maji ya mvua
kazi hapa kibao nimepigwa sumuni mbili
moja ya uji na ingine ya mkate slice mbili
ile part ya fegi, niaje
make sure umecheki m-junior wangu asirande mtaani
by the way Oposh alinyakwa yuko hapa ndani
mpaka saa hii amekataa kunitobokea ni noma gani
kesi inaskizwa baada ya miezi tatu
tutatoka tu ile jaji iko ni mtu wangu
nirudi mtaani tuendelee kufanya mambo

Outro (Jua Cali)
eh, oya, eh chali yangu roll call inaitwa
eh, usipoitika hapa ni noma wacha niende au sio
salimia kila mtu manze
salimia wife
salimia mtoi wangu sana
salimia matha
salimia mbuyu, kila mtu, au sio, baadaye, tuonane jo
eh, noma hapa
ah-ah msinivute hivo
naamka, naamka
naenda, naenda pekee yangu
niacheni niende tu
sawa, sawa, sawa
OK poa

You cannot copy content of this page