Jimwat aka Jimwizzy  – Sitoi Kitu Kidogo Lyrics

Jimwat aka Jimwizzy – Sitoi Kitu Kidogo Lyrics

Intro
Hii track inanichangamsha na vile nilikua nimechoka 
Nimechoka na Kutoa Kitu Kidogo!
Nikipatana na karao tao anani’show atanishika ma’mbao
ka sita Toa Kitu Kidogo

(A Homeboyz Produkshizo na Calif Records)

Chorus
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Unazema nini?!!!”
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Utalala ndani?!!!”
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Mia mbili tu..?”
Ofisa jo! nimechoka na kutoa hongo

Verse 1
Kila mthii anadai corruption ni blunder
ata makarao ,lakini bado wananihanda
napatana nao usiku nikitoka job kwa njia
ka sina mia-mia ,hawezi nihurumia
“Gwanza gijana hebu toa gipande?!!!”
Maze jo huskii nili’isahau afande!
“Oghey!zaza itabidi umelala ndani..!”
Ah!ah! najua rights zangu hio sikubali 
“Eti una rhight..?me nahona una wrong!”
Akanipiga kibao aka’reverse ndai yao
“Hebu wega hii man’gaa gwa mariamu 
inaniongelesha unathani we ni nyanyangu?!!!”
Ah!ah! si hivo, nimefikisha 18 tu juzi 
na kupata I.D ni tafash, si unaelewa kuna upuzi?
ina go-down “Heeebu zlow down 
Zielewi hio lugha, anza guongea ganjiiieh!”

Chorus
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Unazema nini?!!!”
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Utalala ndani?!!!”
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Mia mbili tu..?”
Ofisa jo! nimechoka na kutoa hongo

Verse 2
Tumejazana watu ka 15 kwa hio pick-up,
Kila esto hawakosi watu wa ku’ pick-up!
Ka huna ganji “Beba yeye!”
Nika ni ma’three “Beba yeye!”
Wote wanabonga juu ya thegi anaitwa Onyi
Naskia huko ndani ye ndo ‘First-Body!’
Wanauliza karao “Naskia Onyi hayuko?”
“Hamuna bahati nyang’au Onyi igho!”
Nika kila mtu hapo anatupa mbao
Wanaachiliwa waki’bribe karao na ma’thao
Nikabaki solo sa’ tunaelekea ndani bana
“Umefika nyumbani shugha haraka!”
Akaniambia sina I.D kwa kitabu ya O.B!
Kisha akaongezea ‘Drunk n Disorderly!”
Akakubali amekosea lakini eti hana rubber 
“Naeza futa ukinunua rubber mia saba?!!!”

Chorus
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Unazema nini?!!!”
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Utalala ndani?!!!”
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Mia mbili tu..?”
Ofisa jo! nimechoka na kutoa hongo!

Verse 3
Ndani kunanuka ka’ choo 
Watu wamelala kwa floor 
Fo Fo Fo hadi wana’snore
Najisunda kando nipate ka usingizi
Naskia “Onyi hapa kuna nyama mbichi!”
Kuna giza Ti Ti Ti kuona si eazy
Onyi anabonga, “Kuja hapa chizi!”
Nikithani atanipiga hadi nidedi 
Anazusha, “Hawa mafala wanashika wakidi..?”
Anani’show niketi tukaanza kupiga story,
Eh! Kumbe jela si’ ku’boring?
Napata ma’beste ka’ 52 huko ndani
Mmoja mpaka akaniahidi job mtaani!
Imepita ka’ mwaka tangu hio noma 
Nilipata hio job inanilipa vi’noma
Niko kwa Toyota Prado, nasimamishwa na karao,
Nacheka ka’ mwenda sa’ ile nam’show..;

Chorus
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Unazema nini?!!!”
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Utalala ndani?!!!”
Sitoi Kitu Kidogo!!! ,”Mia mbili tu..?”
Ofisa jo! nimechoka na kutoa hongo

You cannot copy content of this page