Jemimah Thiong’o – Amenipanda Lyrics

Chorus:
Bwana asema, amenipanda mimi
Kando ya mito yenye maji mengi
Bwana asema, amenipanda mimi
Kando ya mito yenye maji mengi

Verse 1:
Ni Bwana alonipanda, kwa mikono yake Baba
Kando ya mito yenye rehema na baraka
Kunipalilia Baba, sikosi mbolea maji
Naishi nikiamini, siwezi nyauka nimepandwa ee

(Chorus)

Verse 2:
Kweli Baba wa rehema, amenipanda mimi
Baraka zanifuata kokote niendako
Amenipa uhai, akalinda afya yangu
Ndiposa nashuhudia, sifa alozipanda Mungu wangu

(Chorus)

Verse 3:
Imani ya wokovu, Hushinda majaribu
Hiyo ni baadhi ya mito nilopandwa kwayo
Mambo yangu yote baba, hupanga kwa utaratibu
Kwa maana anijali, aliyenipanda Mungu wangu wee

(Chorus)

Verse 4:
Hakuna juu mbinguni, wala chini duniani
Anayeshinda Mungu muumba mpanzi wangu
Hunizunguka mimi, kwa damu ya mwanao
Hunilinda vyema, sipati madhara kwani nimepandwa ee

(chorus)

You cannot copy content of this page