Esther Wahome – Hachagui Lyrics

Chorus:
Hachagu kabila, hachagui taifa
Hachagui tajiri, wote awapenda
Hachagu kabila, hachagui taifa
Hachagui tajiri, wote awapenda

Verse 1:
Nilisikia kuna mpenzi ambaye hachagui
wote awapenda, wote awajali
Nilimpa maisha yangu nayo yakawa sawa
Ni mwanaume wa wanaume, hachagui hachagui

(Chorus)

Verse 2:
Nilianza safari kwa mataifa mbalimbali
Ili nitangaze yesu na matendo yake
Wamekubali wamesema yesu ni namba moja
Ni mwanaume wa wanaume, hachagui hachagui

(chorus)

Verse 3:
Natangazia wazee pia na vijana
Kwani huyu mpenzi, hachagui miaka
Hata watoto anasema, wote waje kwake
Ni mwanaume wa wanaume, hachagui hachagui

(chorus)

Verse 4:
Nampenda huyu mpenzi aliyenipenda mbele
Tena alijitoa afe kwa ajili yangu
Damu yake alimwaga ili nisipotee
Ni mwanaume wa wanaume,

(chorus)

Verse5:
Natangaza hachagui, huyu yesu awapenda eh oh
Awapenda wote, huyu yesu
Awajali wote, haleluyah
Awajali wote

(Chorus)

You cannot copy content of this page