DNG ft. Tindi – Iyoo Lyrics

DNG ft. Tindi – Iyoo Lyrics

Intro (DNG)
ladies and gentlemen c-come on
it’s your boy DNG 
introducing the new sensation
Miss Tindi
Jomino of course

Chorus (Tindi)
Iyoo
hii ngoma ni yangu
maisha pia ni yangu
mwelekeo ni yangu
desturi nayo ni yangu

Iyoo 
furaha ni yangu
nakula hepi kivyangu
najivinjari na watu
staarabu nazo ni zangu

Verse 1 (DNG)
Nipe nafasi karatasi na kalamu
wadhii wamepigwa na butwaa kama sanamu
ngoma yashika toka Nairobi hadi Lamu
inaskizwa kanisani jo hata kwa vilabu
na-spit kwa mic na inatoka tu vitamu
ka King Midas yabadilika dhahabu
ajabu kistari imejazwa kitabu
ku-flow nita-flow mpaka mimi niwe babu
kuzaliwa nilizaliwa na ngoma kwa damu
isarasuti wa kale uliza mamangu
vuta kiti keti chini mwanangu
kwani sasa mimi nina hamu na ghamu
kutolea kilicho moyoni mwangu
ili wewe uhisi hisia zangu
furahia tu hii ngoma yangu
verse imeisha wacha chorus ikamu

Chorus (Tindi)
Iyoo
hii ngoma ni yangu
maisha pia ni yangu
mwelekeo ni yangu
desturi nayo ni yangu

Iyoo 
furaha ni yangu
nakula hepi kivyangu
najivinjari na watu
staarabu nazo ni zangu

Verse 2 (DNG)
hi ngoma yangu nitachafua jo 
cheki vile wazeiya nimewakwachu
shika pozi man hebu tulia tu
kidogo tu
nikueleze ilivyokuwa tu
mi ni kijanajana star kipenda raha bana
na waro kizee napenda sana bana
na kutupa mikuki na kulenga bana
na kukula ndazi wembe kuingiana
Jumapili kanisani mi nasali
baadaye nauliza maswali
mbona mi siwezi fanya hivi na hivi
ati kwa sababu haikubaliki
pastor vipi hii story hainibambi
mbona hakuna hata leniency kiasi
sa nitafanyaje na mi nataka ku-party
hii swara
ni dilemma ya mnati

Chorus (Tindi)
Iyoo
hii ngoma ni yangu
maisha pia ni yangu
mwelekeo ni yangu
desturi nayo ni yangu

Iyoo 
furaha ni yangu
nakula hepi kivyangu
najivinjari na watu
staarabu nazo ni zangu

Verse 3 (DNG)
its D to the NG nani kama mimi
I’m down for whatever whenever jo kwani nini
cheki ratili __ swahili
akileta noma papo hapo kumbadili
cheki sato __ akanikaribia
kile alicho nacho jo ananinyuyusia
binti jo unavyong’aa unanipendeza
so huku ni wapi unanipeleka
unanichizisha unavyonipelekesha
mpaka kinywaji nashindwa kuteremsha
temptation kibao unanishikisha
unajua King Solomon umempandisha
situation tricky umeniletea
mpaka nashindwa vipi nitajitetea
wanimaliza nimemalizika
kama mi ni kazi basi nimekamilika

Chorus (Tindi)
Iyoo
hii ngoma ni yangu
maisha pia ni yangu
mwelekeo ni yangu
desturi nayo ni yangu

Iyoo 
furaha ni yangu
nakula hepi kivyangu
najivinjari na watu
staarabu nazo ni zangu

You cannot copy content of this page