Daudi Kabaka – Msichana wa Elimu Lyrics

msichana wa sura nzuri
kitu gani kinakufanya usiolewe

elimu unayo ya kutosha
hata ng’ambo ukaenda ukarudi

msichana wa urembo kama wewe
uonyeshe mapenzi kwa vijana

ukionyesha majivuno kwa vijana
utazeeka ukiwa nyumbani kwenu

ooh baby, miaka yaenda mbio sana
na sura yako nayo ikichuchuka

ooh baby, miaka yaenda mbio sana
na sura yako nayo ikichuchuka

pengine tabia zako ndizo mbaya
awali kweli dada ulijivuna

kwanza mimi nilitaka nikuoe
ukaringa ati sina masomo

ooh baby, ona watoto wa nyuma yako
wameolewa wamekuwacha ukihangaika

ooh baby, ona watoto wa nyuma yako
wameolewa wamekuwacha ukihangaika

msichana wa sura nzuri
kitu gani kinakufanya usiolewe

elimu unayo ya kutosha
hata ng’ambo ukaenda ukarudi

You cannot copy content of this page