Chuma cha Reli – Siku Zangu Lyrics

SIKU ZANGU
Maisha mhudumu , yameleta tofauti na nilichokiagiza
Sahani ya hali ngumu, wakati mwenzenu mi niliomba pizza
Nahisi ni hukumu, huku kutafta pin kwenye giza
Mola simlaumu, najenga imani ipo sku atazusha miujiza
Siku zinakwenda, wenzangu wanachana calendar
Kila nachotenda, hakitoki jinsi nilivyopenda
Nawaza kamba shingoni,ila napoozwa na imani
Nakosa raha moyoni , siku zangu mbona sizioni
Wenzangu naona wakila, kila shoot kwao ni bao
Mwenzao mi napura, shabiki analeta madharau
Nmeishi sana kwenye shinda, kitaani wananiita legendare
Pesa najaribu kuiwinda, ila nabakia kuwa pale pale
Mola nisamehe, nisiwe nimekosa unaniadhibu
Badilisha tarehe, siku zisongeze huku karibu
Ona ngozi imechakaa, sina tena rahaa
Machizi wanishangaa,ila bado sikati tamaa

You cannot copy content of this page