Chuma cha Reli – Nitaoa nikikosa cha kufanya

NITAOA NIKIKOSA CHAKUFANYA
Siko tayari,labda mida ikibadilika
Hili bahari, kuchafuka likome kabisa
Nona hatari, huu mzigo  mpenzi kujitwika 
Mwisho wa safari, niachwe dume mi nasikitika
Sijawa limbuka, nabishana na hizi pepo
Wenzangu nipisheni,najiepusha na hili tendo
Imenishinda, wekeza, kwenye hizi biashara
Natabiri nitateleza, zikanizalie hasara
Niacheni nipotoke,nyi jitoeni kafara
Mtafeli niwaokote, enyi mnaniona kafala
Siogopi majukumu, naogopa kudhulumiwa
Nisitumwe kuzimu,kabla muda niliopangiwa
Walioitana wapenzi, leo wanavuaana mataji
Mi nona hilo siwezi,bara nibaki mtazamaji
Labda nitangoza,baadaye lakini sio leo
Siku mtakaponipoza, mapenzi yana jipya toleo.

You cannot copy content of this page