Chuma cha Reli – Mziki umekuwa p***o Lyrics

MUZIKI UMEKUA p***o?????
Nipende nichukie
Nichekee nifurie
Nikemee nisifie
Mi lazima nikwambie
Kwa jinsi navyoamini mimi
Mie ni tajiri naenzungukwa na maskini
Nkiruhusu wanishauri mnategemea nini?
Kama sio mapeni kunihama mfukoni
Eti nicheze na kahaba stageni
Ndo muziki wangu utaombwa redioni
Mwanamziki bila promo bado mwanamziki
Sio lazima mnisifie ili nijipatie riziki
Mi bado ntachana saana
Usiku,mchana ntakazana
Wakichoka kubana wataachana
Nashangaa muziki umekua kama usingizi wa pono
Wanamziki hawajielewi daily wanatukuza ngono
Media,bila video kuwa kama p***o hakuna promo
Mashabiki shangwe kibao hawajali mnaambukizana kisonono
Umaarufu na mashabiki cjui zimekua ndo nini
Za kuwafanya dada zetu wapande stageni na bikini
Nahesabia siku ukwiro unaawasumbua akilini
Utapungua watakosa ta kujithamini
Haijalishi watakua na mapeni watakua na madini
Najiuliza mbona mkewe msanii hakatiki uchi stageni
Kuparty kila wakati lazima itakua haiwezekani
Labda uwe we ndo shetani ambalo mi sidhani
Nizingatie na ukiona poa unipuuze
Kuwa mrembo haimaanishi lazima ujiuze
Hamjifunzi kutokana na waliowatangulia wanavyodondoka
Hamnihitaji kwa sasa ila ntakuwepo kuwaokota
Sibadililiki mi daima ntaimba ukweli
Fungeni barabara ila mi nasifiri kwa meli
Nipende nichukie
Nichekee nifurie
Nikemee nisifie
Mi lazima nikwambie

You cannot copy content of this page