Chuma Cha Reli – Kwenu kuna stima Lyrics

KWENU KUNA STIMA
Kwenu Kuna Stima 
Kila Usiku wa jana upitaa,
Unaniacha Mwenzenu na Mziga kibao,
Mzigo wa hasira Moyoni Ninao
Japo kila kuchao najilazimisha kusahau
Wakifanya vinywa vyao wadau
Hawafanyi lolote zaidi ya kunikumbusha
Mimi ndo kitoweo chao
Natumika kama mpira sababu
Maishani sina dira
Naamini aliyeniambukiza huu ujinga
Ana uhusiano na mganga anayetaka kuniganga
Utaniambiaje wakimwaga mboga nimwage ugali
Wakati chakula chao ni maziwa na asali
One, two, one, two, wanaenda vipazo
Wakisubiri giza limeza mwangoza
Ili vifo vyetu waje kuvitangaza
Ajabu naogelea kwenye damu bila kujali
Alichinjwa nani nikielezwa marehemu
Alinitanguliza nataka kubisha haiwezekani
Mwanasiasa hivi we umetumwa na nani?
Mbona uwe kama balozi wa Shetani?
Vijana imewashinda kutumia bongo zao
Kwetu kuna giza kibao.

You cannot copy content of this page