Chuma cha Reli – Kubali imekushinda usaidiwe Lyrics

KUBALI IMEKUSHINDA USAIDIWE
Mi naskia skia tu!
Eti maisha kama kioo ukiyachekea yanakuchekea,
Nimejaribu kucheka kwenye msiba ,sipendi picha ilivyotokea
Cameraman kutuamuru tutabasamu ili atupige picha,
Haibadili chohote, itafahamika tu kuna kitu tulificha.
Sishabikii saaana zile ndoto za kitandani,
Maana nimeota mengi, mengi ambayo hayawezekani.
Nataka kuishi kwenye uhalisi wa dunia,
Ambapo ukijingonga kwenye ukuta unaumia.
Tofauti kabisa na kitu mnachoniambia.
Kila siku eti “the party don’t stop”.
Wakati katika uhalisia tunastruggle kucope.
Maskini akijitita bill gate A.K.A tajiri,
Asitegemee msaada wowote wa kimali
Najua maneno yangu yanaonekana kama propaganda,
Lakini sioni ujanja wowote kuenda club na hela ya msiba.
Sisemi tuomboleze kwenye harusi,
Nasema usimeze A.RV kama huna virusi.
Africa kuna umaskini.
Kama sio kwako basi kwa jirani.
Tumeendelea maana si dada zetu wamejua vimini?
Na pia tunatongozana kwa simu za mkononi?
Lakini wenzetu wanateseka ina maana hawamwoni?
Kujiita tajiri haina maana endapo utakosa kitu mfukoni
Sijali nitawapotezza marafiki lolote na liwe.
Ishi kihalilisia ,kumbali una shinda usaidiwe.
By chuma cha reli

You cannot copy content of this page