Chuma cha Reli – Hakuna mapenzi Lyrics

Hakuna mapenzi
Bora nitapeliwe, ila siwezi jitapeli
Binadamu anajiita jiwe, ishara sio mkweli
Hakuna mapenzi, labda ukwiro na tama
Pressure ya wazazi, na kutamani kuzaa
Mi nona nkivua jezi, aki ya nani mi sichezi
Hili ni gemu la wezi, mwisho itakuja kuwa kesi
Waliopeana ubikra, leo wanatatizika kifikra
Sipendekezi hata subra, naona poa kuishi tu’bla
Hakuna mpenzi, labda kwenye nyimbo
Majarida ya mwisho wa mwezi, na kwenye tungo
Unachokifanya ki-enzi, usipoteze muda wako
Kiwekeza kwenye mapenzi, hasara ndo zako
Pingana na mie, ukiona poa nichukie
Ninunie, ila yakikutokea mwenzako sinililie
Najua haiwezekani, watoto kununuliwa dukani
Wala sipingani, na ulichofunzwa kanisani
Unahitaji mwandani, ila asiwe kama kileo
Umweke ndani, ili jamii ikupe cheo
Sijakuona siwezi lala, ni tungo za kifala
Mapenzi ni biashara, na kujitoa kafara
Nifaidi nikufaidi, ndo lengo la mapenzi
Nikiita biashara unakaidi, yako wapi mapenzi?
Mi najiweka pembeni, nyi chezeni
Mi ntakazana kuchana, nijipatie mapeni
Nyi chumbianeni kwa saana, mjipatie madeni
Nitaoa siku moja ikiwezekana, ila sio kwa yangu hisani//wanangu

msiniombee laana, ni mapenzi ndo hayapatikani.

You cannot copy content of this page