Chuma cha Reli – Facebook City Lyrics

FB CITY:
Vijana wa jana na enyi wana mnaokazana
Kufurahishana na kutongozana na watu msiojuana
Ana kwa ana ,Nawasalimu saana maaana sio juzi
Wala jana tumeonana
Siku mnahamia mjini nilijilazimisha kuamini
Hazitapita siku ishirini hamjarudi kijijini kuwa na mimi
Lakini mjini kama baharini mmezamia kwa ndani hampatikani
Baba na bibi wanalalamika eti mmewatenga
Wanasimulia hadithi na ni nyinyi wanawalenga
Hawajaweza kuamini wajukuu wamewapiga chenga
Wanauliza mtarudi lini au mnasubiri kipenga?
Najua mtaniona kama mhuni niliyevamia game
Lakini tangu mmeenda mjini life lenu sio tena the same
Mmetoa usingizi kafara,usiku kucha naskia hakuna kulala
Mnasafiri sana ila bila daladala ,Na si hatujaja mjini mnatuita mafala
Nasikia facebook ni mjini kweli,kuna wanaojiuza na kuna matapeli
Kuna ajali japo sio za magari na biashara za halali
Makundi mbalimbali,mengine ya hali na mengine ya hatari
Lipo Sana awala la copy and paste na wenye nacho wanadaiwa sana ubeshti
Sikusoma kama mnazinguana na kutongozana mkinyanganyana
Mabwana na wengine kutishiana kuuana
Nimejulishwa mimi huko mjini kuna waumini wanaosambaza dini
Lakini asilimia tisini hawatalii makini maswala ya amani lao ni
Burudani na kutamani maisha ambayo hayawezekani
Nasikia tena eti,Lakini wacha niache kuandika mengi
All in All nakazana sana kuona kama itawezekana kuonana
Kabla mji ukue sana tutaonana ni mimi wako mwana;
Chuma cha reli motto mgumu saana

You cannot copy content of this page