Chuma cha Reli – Bunge la Vijiweni Lyrics

BUNGE LA VIJIWENI
Kwa kutizama tu bila kufikiri utadhani ni wanaharakati
Waliopewa viti vya thamani ila wakaamua “hatuvitaki”
Walichanguliwa na nani, wanawakilisha nani, haijulikani
Au ndo hawana majukumu kwao manyumbani?.
Mara ooh! Wanawake ndo hutulia majumbani,
Mara ooh! Lazima nichill na masela kitaani.
Mara ooh! Si unajua kazi ndo hazipatikani 
Mh!
Sibishi! Vijiweni kuna kazi!
Kazi ya kujadili magari yanayokwenda kwa kasi,
Mshahara anaoingiza lionel messi kila mwezi,
Bila kusahau ile ya kuwalea majambazi.
Si unaona wanatoa na kuinua vipaji?
“Bungeni” hawajadili jinsi ya kuizusha dollar.
Wanajadili njia bora za kutupora.
Watoto wadogo watawashinda hata kureason,
Wana ndoto za kutajirika ati wakiwa freemason.
Wanaongoza kwa kutongoza,
Wanaongoza kwa kupotosha.
Baya zaidi mijadala yao haiwalipi.

You cannot copy content of this page